8 Februari 2026 - 12:51

Jumuiya ya Kiislamu ya Bangladesh imetoa tamko rasmi ikitangaza uungaji mkono wake kamili kwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, na kuonya kuwa shambulio lolote la kijeshi dhidi ya Iran litakabiliwa na mwitikio mpana wa Waislamu duniani. Katika tamko hilo imesema: “Ingawa viongozi wa baadhi ya nchi za Kiislamu wanategemea Marekani na Israel, lakini Waislamu bilioni mbili duniani wamesimama pamoja na Palestina. Ikiwa uvamizi wa kijeshi utafanywa dhidi ya Iran, Waislamu kote duniani wataingia uwanjani kwa mali na nafsi zao; na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel utaanguka hivi karibuni.”

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA- Jumuiya ya Kiislamu ya Bangladesh katika taarifa yake imesisitiza kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa zaidi ya miongo mitano imekuwa ikiunga mkono daima Wapalestina wanaodhulumiwa.

Tamko hilo pia limegusia mauaji ya hivi karibuni ya viongozi kadhaa wa kisiasa na kijeshi wanaounga mkono Palestina katika nchi za Lebanon, Iraq, Yemen, Palestina na Iran, likibainisha kuwa Marekani na utawala wa Kizayuni walidhani kwa vitisho na njama za kumuua Ayatullah Khamenei, harakati za ukombozi wa Palestina zingekoma kabisa, lakini dhana hiyo ni potofu kabisa.
Jumuiya hiyo iliongeza:

“Ingawa baadhi ya viongozi wa nchi za Kiislamu ni wategemezi wa Marekani na Israel, lakini Waislamu bilioni mbili duniani wamesimama upande wa Palestina. Ikiwa shambulio lolote dhidi ya Iran litafanyika, Waislamu kote duniani watajitokeza kwa mali na nafsi zao, na kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, utawala wa Kizayuni wa Israel utaanguka.”

Tamko hilo limetolewa wakati Jumuiya ya Kiislamu ya Bangladesh iliandaa maandamano ya amani baada ya Swala ya Ijumaa mbele ya lango la kaskazini la Msikiti wa Kitaifa wa Baitul-Mukarram. Mkusanyiko huo ulikuwa ni wa kupinga mipango ya uvamizi wa kijeshi wa Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran pamoja na vitisho vya kumuua Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Katika hafla hiyo, pamoja na Maulana Abu Swaleh, pia walihutubia Maulana Issam Abdul-Hamid, Maulana Khairul-Islam, Maulana Abul-Khair, Maulana Mutawal Hussein na wengineo.

Maulana Issam Abdul-Hamid alisema kwa kunukuu Hadithi ya Mtume (saw):
“Umma wa Kiislamu ni kama mwili mmoja. Popote Waislamu wanaposhambuliwa duniani, nasi tutasimama na kupinga.”

Pia akirejea historia ya vita vya mwanzo wa Uislamu, alisema:
“Katika zama za Mtume Muhammad (saw), Mayahudi walishindwa vitani na wakafukuzwa Khaybar.”
Akaongeza:
“Israel ya leo inatafuta kuanzisha Israel kubwa zaidi. Wanataka kuiteka Syria, Iraq na hata Madina. Lakini ikiwa Waislamu wataungana, hawatakuwa na njia ya kutoroka.”

Tags

Your Comment

You are replying to: .
captcha